Kwa mujibu wa idara ya tarjama ya SShirika la Habari la Hawza, hatua hii ya pamoja imeandaliwa na Muungano wa Kimataifa kwa ajili ya Palestina, kwa uungwaji mkono na Harakati ya Kupinga Apartheid (AAM) pamoja na Muungano wa Kimataifa dhidi ya Uvamizi wa Palestina (SANED). Hatua hiyo inalenga kuanzisha uingiliaji wa kiraia uliounganishwa na wa moja kwa moja, kwa lengo la kukomesha ushirikiano wa umma na kudai uwajibikaji wa kimfumo dhidi ya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu unaofanywa na utawala wa Israel. Siku hii ya kimataifa ya hatua inakusudia kuleta pamoja aina tofauti kabisa ya uhamasishaji wa umma chini ya mfumo mmoja wa kimataifa wa pamoja.
“Uhamasishaji wa tarehe 10 Oktoba” utaunganisha harakati ambazo tayari zimejipanga kwa ajili ya Palestina katika nchi zao, na kuzipa mfumo wa pamoja ambao mashirika yataweza kuutumia kuchukua hatua kwa namna inayozingatia mazingira yao ya kisiasa na kijamii. Hatimaye, mpango huu utazileta pamoja kampeni za ndani kupitia wikendi moja ya kimataifa iliyoratibiwa kwa pamoja.
Uhamasishaji huu umejengwa juu ya miito miwili mikuu: kutetea ardhi na kukomesha mauaji ya kimbari. Miito hiyo inashughulikia mashambulizi yanayoendelea ya Israel dhidi ya Ghaza, pamoja na kuongezeka ghasia zinazofanywa na walowezi wanaoungwa mkono na serikali, uporaji wa ardhi na mashambulizi ya kijeshi katika maeneo yote ya Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu.
Chanzo: MIDLE EAST MONITOR
Maoni yako